NEWALA, MTWARA
Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya wilaya ya Newala, Ndugu Duncan Thebas amekutana na Viongozi wa dini, Siasa na Wazee katika kikao cha kutoa maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri.
Thebas ametumia kikao hicho kuwapa taarifa wananchi kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika Novemba 27,2024 siku ya jumatano na kazi ya uandikishaji wa wapiga kura utafanyika tarehe 11-20 Oktoba 2024 kuanzia saa 2.00 asubuhi mpaka saa 12 jioni ,ambapo kazi hiyo itafanyika katika vitongoji vyote 302 katika vijiji 107 vilivyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Newala.
Aidha kutokana na umuhimu wa uchaguzi huu,amewahimiza Viongozi wa dini,siasa na wazee walioshiriki kikao kwenda kuhamasisha wakazi wote wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura na kushiriki uchaguzi kwa amani ili kuwapata viongozi bora.
"Tanzania ni kisiwa cha amani,nendeni mkahamasishe wananchi kujiandikisha na kushiriki uchaguzi pamoja na kulinda amani na usalama wa nchi hii" amesema Thebas.
Msimamizi Duncan Thebas amewahakikishia Viongozi wa siasa kuwa atasimamia na kuhakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa 27,2024 unafanyika kwa kufuata mwongozo wa uchaguzi ambao umefafanua taratibu na kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika ngazi za msingi.
@ortamisemi
@mtwarars_habari
@dc_newala
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa