Mkuu wa Wilaya ya Newala, Mhe. Aziza Mangosongo amefungua rasmi mafunzo ya watoa huduma ngazi ya jamii (LSPs) tarehe 02/01/2018 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Akizungumza katika ufunguzi huo, Mhe. Mangosongo amewataka wasimamizi hao wa miradi kuwa wazalendo kwa kusimamia vema miradi hiyo na kutoa ushauri wa kitaalamu pale unapohitajika ili kuleta ufanisi katika miradi husika.
Mbali na kusimamia miradi hiyo, Mhe. Mangosongo amewataka wasimamizi hao kusikikiliza na kusaidia kutatua kero za walengwa pale inapowezekana kwa kuwa sasa wao wanaufahamu mpango vizuri pia kuwahamasisha walengwa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) kwa kuwa itawasaidia katika kupata huduma za matibabu wao na familia zao.
Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Mussa Chimae akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya watoa huduma ngazi ya jamii kwa miradi ya TASAF
Mafunzo hayo yalitolewa kwa wasimamizi wa miradi kwa vijiji 97 vya Wilaya ya Newala vilivyopo kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini na yalichukua muda wa siku 6 kuanzia tarehe 02/01/2018 hadi tarehe07/01/2018.
Miradi hiyo inatarajiwa kutekelezwa kuanzia mwezi Januari hadi Aprili 2018, na ni jumla ya miradi 102 katika vijiji 97 vilivyopo kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini na itakuwa na jumla ya Tsh. 949,078,043.00
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa