Watumishi wa ajira mpya kwa Halmashauri ya Wilaya ya Newala, jana tarehe 23/04/2021 wamepewa mafunzo maalum ya kiutumishi ili kuelewa mazingira wanayofanyia kazi.
Watumishi wapya wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala wakisikiliza mada zilizowasilishwa katika kikao kazi cha mafunzo ya awali kazini kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha walimu Kitangari.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha ualimu Kitangari ambapo watumishi hao walielekezwa kuhusu maadili ya Utumishi wa umma; misingi ya sheria katika kusimamia haki na wajibu kwa watumishi wa umma; miongozo na sera mbalimbali ya kuifuata katika utendaji wao wa kazi na namna bora ya kudumisha mahusiano mazuri katika maeneo yao ya kazi na watu wanaowatumikia.
Mafunzo hayo yalifunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Duncan Thebas na yaliendeshwa na Afisa Utumishi na utawala, Katibu wa tume ya Utumishi ya walimu, Afisa Elimu Msingi, Afisa Elimu Sekondari, Mthibiti na Mkaguzi ubora wa shule pamoja na Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania Wilaya ya Newala.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa