Halmashauri ya Wilaya ya Newala inaadhimisha wiki ya chanjo kuanzia Jumatatu tarehe 24 mpaka tarehe 30 Aprili 2017. Hii ikiwa ni kwenda sambamba na maadhimisho ya chanjo kitaifa. Maadhimisho haya yatahusisha utoaji wa chanjo kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano na wanawake wote wenye umri wa kuzaa kuanzia miaka 19 hadi 49. Chanjo hizo zinatolewa bila malipo katika vituo vyote vya huduma za afya na kwenye maeneo ambayo yapo mbali na vituo vya kutolea huduma hizo. Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Newala uzinduzi utafanywa na waheshimiwa madiwani katika kata zao na kiwilaya uzinduzi rasmi utafanywa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Aziza Mangosongo katika kituo cha Afya cha Kitangari. Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Chanjo hukinga kila mtu, pata chanjo"
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa