Wajumbe wa kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Newala leo tarehe 14/05/2020 wamefanikiwa kutembelea miradi sita inayoendelea kutekelezwa.
Miradi hiyo ni Ujenzi wa madarasa matatu na ofisi moja ya walimu katika shule shikizi ya Chikuti, ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Nandwahi, ujenzi wa shule shikizi katika kijiji cha Mpirani, maandalizi ya eneo la ujenzi wa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Newala katika kijiji cha Mchemo na ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Mpwapwa.
Kamati hiyo iliongozwa na Mhe. Chitwanga Rashid Ndembo, mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala na diwani wa kata ya Mtunguru.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa