• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Newala District Council
Newala District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Newala

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko
      • Ukubwa wa eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya viongozi
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ujenzi
      • Planning, Statistics and Coordination
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • KIlimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • ICT & Public Relations
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Usambazaji
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
      • TASAF
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba

Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Newala lafikia ukomo

Posted on: June 9th, 2020

Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Newala leo tarehe 09/06/2020 limefikia ukomo rasmi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala  Bw. Mussa Chimae akiwasilisha taarifa katika mkutano maalum wa kusitisha shughuli za baraza la madiwani leo tarehe 09/06/2020.

Akiwasilisha taarifa yake katika mkutano huo maalum wa kusitisha baraza la madiwani, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bw. Mussa Chimae amesema kuwa madiwani hao waliingia rasmi madarakani tarehe 25/10/2015 na baraza linaahirishwa leo ili kupisha mchakato mwingine utakaowapata madiwani wengine kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025. Hivyo majukumu yote ya baraza hilo wakati madiwani hawapo yatafanywa na menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Newala na maamuzi yote yatatolewa taarifa katika baraza la madiwani lijalo litakaloundwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo akizungumza katika mkutano  maalum wa kusitisha shughuli za baraza la madiwani leo tarehe 09/06/2020 katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha walimu Kitangari. 

Akizungumza katika mkutano huo maalum wa kuahirisha shughuli za  baraza la madiwani, Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo amelipongeza baraza hilo kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mhe. Mangosongo amewaeleza madiwani kuwa wakati wanatekeleza majukumu yao kwa kushirikiana na wataalamu, walikuwa wanatekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.

"Tuna kitabu cha ilani ya Chama cha Mapinduzi kinachoelezea kila sekta na mambo yatakayotekelezwa na asilimia za utekelezaji wake, hivyo yote yaliyokuwa yanatekelezwa yamefuata maelekezo hayo." Amesema Mhe. Mangosongo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Mhe. Chitwanga Rashid Ndembo akifunga mkutano maalum wa kusitisha shughuli za baraza la madiwani

Akifunga mkutano huo maalum wa kusitisha shughuli za baraza la madiwani, mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Mhe. Chitwanga Rashid Ndembo amewashukuru waheshimiwa madiwani na watumishi wote kwa imani yao kwake na ushirikiano waliompa kwa muda wote madiwani walipokuwa madarakani na amewataka kuendelea kufuata sheria, taratibu na kanuni katika kila watakachokuwa wanakifanya.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -HALMASHAURI YA WILAYA YA NEWALA December 29, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILII WA MAHOJIANO January 06, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2021 MNYAMBE SEKONDARI July 10, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 22, 2022
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • NEWALA DC YATEKELEZA MPANGO WA TASAF KWA MAFANIKIO MAKUBWA

    July 17, 2025
  • MWEZI WA AFYA NA LISHE KWA WATOTO

    July 04, 2025
  • UJUMBE WA SHUKRANI KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    July 04, 2025
  • NEWALA DC YAPOKEA MITUNGI YA GESI

    June 24, 2025
  • Ona Zote

Video

Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Historia ya Halmashauri
  • Idara ya Rasilimali Watu

Kurasa mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Poralg
  • Secretariet ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Kitangari,Newala

    Anuani ya Posta: P.O. Box 16

    Simu: +255232410251

    Mobile:

    Barua pepe: ded@newaladc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma zetu

Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa