Monday 2nd, December 2024
@NEWALA DC
MWENYEKITI WA HALMSAHAURI YA WILAYA YA NEWALA MH. MFAUME T. LADA LEO TAREHE 12/07/2023 AMEKABIDHI ZAWADI YA PIKIPIKI AINA YA TVS KWA WATENDAJI WA VIJIJI VINNE(4) VILIVYOFANYA VIZURI KATIKA MAKUSANYO YA MAPATO YA HALMASHAURI KWA MWAKA WA FEDHA 2021/2022 ZENYE THAMANI YA SHILINGI 11,400,000/=
AIDHA PIKIPIKI HIZO ZIMEKABIDHIWA KWA VIJIJI VYA KITANGARI HOSPITALI,MPWAPWA,NAMBALI NA KIJIJI CHA MAKUKWE.
ZOEZI LA MAKABIDHIANO HAYO YAMESHUHUDIWA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NEWALA NDUGU DUNCAN G. THEBAS,WAKUU WA IDARA NA VITENGO,WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI PAMOJA NA WATUMISHI MBALIMBALI.
PIA KUTOLEWA KWA ZAWADI HIZO NI MWENDELEZO WA MKAKATI WA HALMASHAURI KUTOA MOTISHA KWA WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI ILI KUCHOCHEA UKUSANYAJI WA MAPATO YA HALMASHAURI.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa