MTWARA
Halmashauri ya wilaya ya Newala imepata cheti cha pongezi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa katika mbio za mwenge wa uhuru za mwaka 2023.
Cheti hicho kimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kan. Ahmed Abbas katika kikao cha kwanza cha maandalizi ya mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2024 kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara,Machi 7,2024 na kuhudhuriwa na wakuu wa wilaya, wenyeviti wa Halmashauri, Makatibu Tawala, Waratibu wa mbio za mwenge , wawakilishi na viongozi wa chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara.
Halmashauri ya wilaya ya Newala imeshika nafasi ya kwanza kwa kupata Alama za vigezo za jumla 78.18 ikifuatiwa na Nanyamba TC alama 76.70, Newala TC alama 75.85, Masasi TC alama 75.25, Tandahimba alama 74.88, Masasi DC alama 74.67, Mtwara DC alama 72.70, Nanyumbu alama 71.47 na Mtwara MC alama 62.00.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa