Mbunge wa Jimbo la Newala vijijini Mhe. Maimuna Mtanda leo January 02, 2025 amekabidhi kompyuta 10 katika shule ya Sekondari Nanda iliyopo kata ya Muungano Halmashauri ya wilaya ya Newala ili ziwasaidie wanafunzi kujifunza somo la TEHAMA
Akikabidhi kompyuta hizo Mhe Mtanda ameishukuru serikali na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa Dkt.Stergomena Tax ambaye aliahidi kutoa Kompyuta hizo wakati alipofanya Ziara na kuzindua shule hiyo baada ya kupokea maombi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Newala vijijini Mhe.Maimuna Mtanda .
Aidha Mhe Mtanda amewaasa wananchi wa kata ya Muungano kuiunga mkono serikali na chama cha mapinduzi kwani serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia imekuwa ikitatua kero za wananchi na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wakati.
Sambamba na hilo katika kuunga mkono jitihada za serikali katika suala la elimu Mhe Mtanda pia amekabidhi rimu za karatasi kwa ajili ya shughuli za ofisi na Mipira miwili katika shule hiyo ili iwasaidie kukuza michezo.
Kwa upande wa Afisa Takwimu Elimu ya sekondari Ndugu Salumu Mnuwone ambaye alipokea kompyuta hizo kwa niaba ya Mkurugenzi amemshukuru Mbunge Mtanda kwa kufanikisha upatinaji wa Kompyuta hizo na kazi nzuri ya kuchochea maendeleo katika Halmashauri ya wilaya ya Newala.
@ortamisemi
@msemajimkuuwaserikali
@mtwarars_habari
@dc_newala
@s.l.tax
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa