Halmashauri ya Wilaya ya Newala siku ya Jumatano tarehe 02/10/2019 imepongezwa kwa kufanya vizuri katika utekelezaji wa miradi saba (7) iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru.
Pongezi hizo zimetolewa na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bw. Mzee Mkongea Ali wakati wa kuhitimisha mbio hizo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Newala na kuendelea kwenye Halmashauri ya Mji wa Newala siku ya Alhamisi tarehe 03/10/2019.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Bw. Mzee Mkongea Ali akizungumza na wana Newala katika eneo la mkesha wa Mwnge wa Uhuru siku ya Jumatano tarehe 02/10/2019.
Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Newala, Mwenge wa Uhuru umekimbizwa katika umbali wa kilomita 81.2 kwenye kata 9, vijiji 17 na umepitia miradi 7 yenye thamani ya shilingi 1,390,623,555 ambapo mradi mmoja umewekwa jiwe la msingi, miradi mitano imeonwa na kukaguliwa na mradi mmoja umezinduliwa.
Miradi hiyo ni ujenzi wa bweni moja, madarasa mawili na ununuzi wa samani katika shule ya sekondari Mnyambe, uzinduzi wa klabu ya uchaguzi katika kijiji cha Mnyambe, kuona na kukagua maendeleo ya klabu ya kupinga rushwa shule ya sekondari Mnyambe, kuona na kukagua huduma za afya zinazotolewa katika Halmashauri ya Wilaya ya Newala, mradi wa maji na kupanda miti chanzo cha maji mitema, shughuli za vikundi vya wajasiriamali wanawake, vijana na walemavu, na ukaguzi wa mabanda ya TAKUKURU, Polisi, uchaguzi na afya.
Mwenge wa Uhuru kwa Halmashauri ya Wilaya ya Newala ulipokelewa katika kijiji cha Miyuyu na kukesha katika kijiji cha Kitangari ukiwa na kauli mbiu isemayo "Maji ni haki ya kila mtu, Tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa"
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa