Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Mussa Chimae kwa kuwajali na kuwawekea mazingira mazuri ya kufanyia kazi walimu wote wanaoripoti kufanya kazi katika shule zilizopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Mhe. Majaliwa aliyazungumza hayo siku ya Jumanne tarehe 27/02/2018 alipofanya ziara yake ya kawaida ya kikazi katika Wilaya ya Newala na kutembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa chuo cha ualimu Kitangari.
Akizungumza na wananchi wa Kitangari, walimu, wanafunzi na watumishi wa Halmashauri, Mhe. Majaliwa alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala kwa mazingira mazuri anayowawekea walimu kwa kuwawezesha vyakula, malazi, fedha za kujikimu na usafiri wa kufika kwenye vituo vyao vya kazi pindi wanaporipoti kufanya kazi kwenye shule zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Mhe. Majaliwa alisema kwa kutoa huduma hizo kunamfanya mwalimu husika ajisikie vizuri na aanze kufanya kazi kwa ari kwa kuwa ana uhakika wa kuanza maisha vizuri. Hivyo Mhe Majaliwa aliwataka Wakurugenzi wote kuiga mfano huo kwa kuwa utasaidia kuwafanya walimu wafanye kazi kwa ari na kukubali mazingira yoyote.
Ziara hiyo ilikuwa ya siku moja na ilihusisha kuongea na watumishi na kuwakumbusha wajibu wao kwa jamii, kutembele na kukagua ujenzi unaoendelea wa chuo cha ualimu Kitangari na kuongea na wananchi wa Newala katika uwanja wa sabasaba.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa