• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Newala District Council
Newala District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Newala

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko
      • Ukubwa wa eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya viongozi
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ujenzi
      • Planning, Statistics and Coordination
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • KIlimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • ICT & Public Relations
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Usambazaji
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
      • TASAF
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba

Wanawake wa Wilaya ya Newala waadhimisha siku ya mwanamke duniani kwa kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa

Posted on: March 8th, 2019

Wanawake wa Wilaya ya Newala waadhimisha siku ya mwanamke duniani tarehe 8 mwezi Machi kwa kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa katika kituo cha afya Kitangari.

Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Newala Ndugu.  Daniel Zenda ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Newala Bi. Aziza Mangosongo.


Ndugu. Zenda akimjulia  na kumpatia mahitaji mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika kituo cha afya Kitangari, Halmashauri ya Wilaya ya Newala.

Ndugu. Zenda aliwaongoza wanawake wa Newala kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa ambapo wagonjwa hao walipewa mahitaji mbalimbali yakiwemo sabuni za kuongea na kufulia, maji ya kunywa pamoja na juisi. Pia kituo cha afya kilipatiwa sabuni kwa ajili ya kufanyia usafi.

Akizungumza na wananchi wa Kitangari na wanawake wa Newala kwa ujumla baada ya zoezi la kuwafariji wagonjwa,  Ndugu. Zenda ameahidi kuwatafutia ufumbuzi wa upatikanaji wa masoko ya bidhaa za wajasiriamali wa Newala pia amewataka wanawake kuthubutu na kutochagua kazi.


Katibu Tawala wa Wilaya ya Newala Ndugu. Daniel Zenda (aliyesimama)  akizungumza na hadhara iliyojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani kata ya Kitangari, Halmashauri ya Wilaya ya Newala.

Akiendelea kuzungumza, Zenda amezipongeza Halmashauri zilizopo Wilaya ya Newala kwa kujitahidi kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake hivyo kuwafanya kuwajibika na amezisisitiza Halmashauri kuendelea kutoa mikopo hiyo kwa vikundi vingi zaidi.

Ndugu. Zenda akikagua bidhaa za biashara za wajasiriamali wa Newala kwenye maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani.

Maadhimisho hayo yaliambatana na maonesho ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na vikundi vya wanawake wajasiriamali; maonesho ya sanaa za ngoma za asili, muziki wa kizazi kipya, maigizo na michezo mbalimbali ikiwemo kukimbia na vijiko mdomoni vikiwa na mayai,kukimbia kwa kuvaa magunia miguuni na kuvuta kamba.

Baadhi ya wanawake waliohudhuria maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani wakishiriki mchezo wa kukimbia wakiwa wamevaa magunia miguuni. 


Kila mwaka tarehe 8 mwezi Machi ni maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani ambapo kwa mwaka huu 2019, kwa Wilaya ya Newala,  maadhimisho hayo kiwilaya yamefanyika katika kata ya Kitangari na kauli mbiu ni "Badili fikra kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu".

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -HALMASHAURI YA WILAYA YA NEWALA December 29, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILII WA MAHOJIANO January 06, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2021 MNYAMBE SEKONDARI July 10, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 22, 2022
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • RAIS SAMIA AMEBORESHA SEKTA YA ELIMU NEWALA DC

    March 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA KINYWA NA MENO WAHUDUMIA WAGONJWA 319 NEWALA DC

    March 24, 2025
  • MIAKA 4 YA RAIS DKT. SAMIA SALUHU HASSAN AMEBORESHA HUDUMA ZA AFYA

    March 19, 2025
  • NEWALA DC YANUFAIKA NA JENGO LA UTAWALA,WATUMISHI

    March 18, 2025
  • Ona Zote

Video

Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Historia ya Halmashauri
  • Idara ya Rasilimali Watu

Kurasa mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Poralg
  • Secretariet ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Newala

    Anuani ya Posta: P.O. Box 16

    Simu: +255232410251

    Mobile:

    Barua pepe: ded@newaladc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma zetu

Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa