Naibu waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mwita Waitara amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Newala siku ya Jumamosi tarehe 09/03/2019.
Akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri mbili za Wilaya ya Newala katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala, Mhe. Waitara alisema kuwa, lengo la kikao chake na watumishi ni kuwakumbusha wajibu walionao na kazi wanazotakiwa kufanya.
Akiendelea kuzungumza na watumishi hao, Mhe. Waitara amewataka kila mtumishi kwa nafasi yake atimize wajibu wake kwa kuwa Wizara ya TAMISEMI na Serikali kwa ujumla wanawategemea sana watumishi katika utendaji kazi wao.
Mhe. Waitara pia amewataka watumishi kutokufanya kazi kwa mazoea na viongozi kutokuwaonea watumishi katika utendaji wao wa kazi bali pale inapobidi kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya mtumishi basi ifanyike hivyo.
Ziara hiyo ya naibu Waziri wa TAMISEMI ilihusisha kutembelea miradi inayotekelezwa katika sekta ya elimu na kuzungumza na watumishi wa umma wote waliopo Wilaya ya Newala.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa