NEWALA, MTWARA
Afisa Uchaguzi Halmashauri ya wilaya ya Newala Ndugu Lukumbuso John Mbwilo amesema vituo 302 sawa na vitongoji 302 katika Halmashauri ya wilaya ya Newala vitatumika uandikishaji na kupiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika 27,Novemba 2024
Mbwilo amesema hayo leo Agoati 21,2024 wakati akihojiwa na Afisa Habari wa Newala DC ofisini kwake kuhusu umuhimu na maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.
"Umuhimu wa kuchagua viongozi wa serikali za mitaa ni kupata viongozi wenye sifa ambao wanajua maana ya maendeleo kwa wananchi kwa sababu katika ngazi ya chini wao ndio wanasimamia fedha za serikali zinazotumika kujenga miradi ya maendeleo"
" Tuchague viongozi imara,bora na makini kwa ajili ya kuleta maendeleo katika vijiji vyetu " amesema Mbwilo.
Aidha ametoa wito kwa wananchi wenye umri kuanzia miaka 18 kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha kuwa mpiga kura litakapoanza zoezi la uandikishaji Oktoba 11,2024 mpaka Oktoba 20,2024 na kuhudhuria mikutano ya kampeni ili kupima nani anafaa kuwa Kiongozi wa Serikali ya Kijiji au Kitongoji .
@ortamisemi
@samia_suluhu_hassan
@dc_newala
@mtwarars_habari
@patricksawala
@msemajimkuuwaserikali
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa