Halmashauri ya Wilaya ya Newala leo tarehe 27/05/2020 imepatiwa vitambulisho 1200 vya wajasiriamali wadogo wadogo.
Vitambulisho hivyo vimetolewa mbele ya Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Newala Bi. Aziza Mangosongo ikiwa ni muendelezo wa zoezi la uuzaji wa vitambulisho hivyo lililoanza mwezi Januari 2019 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Newala Bw. Lucas Luoga akikabidhi vitambulisho vya wajasiriamali 1200 kwa Afisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bi. Tumaini Saidi
Akizungumza katika zoezi hilo la ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali, Mhe. Mangosongo amewataka wajasiriamali wadogo kufika katika ofisi za vijiji na kata kuchukua vitambulisho hivyo kwa gharama ya shilingi elfu ishirini tu.
"Vitambulisho hivi vya wajasiriamali wadogo vinasaidia sana kwa kuwa ukilipa elfu ishirini tu utadumu na kitambulisho hicho kwa mwaka mzima na hutadaiwa ushuru wa Halmashauri wala kubughudhiwa na mtu yoyote." Amesema Mhe.Mangosongo.
Watendaji wa kata na vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala wakiapa kiapo cha uaminifu na uadilifu kabla ya kukabidhiwa vitambulisho vya wajasiriamali kwa ajili ya kuviuza.
Zoezi hilo la uuzaji wa vitambulisho vya wajasiriamali litafanywa na watendaji wa kata na vijiji ambao leo wameapa kiapo cha uaminifu na uadilifu katika kusimamia zoezi hilo.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa