NEWALA, MTWARA
Madaktari Bingwa 6 wa Mama Samia wameanza kambi septamba 17,2024 katika Kituo cha Afya Kitangari kwa ajili ya kutoa huduma za Afya kwa Wananchi.
Madaktari hao Bingwa wamepokelewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Dkt George Matiko ikiwa ni awamu ya pili ya muendelezo wa Rais Samia kujali Afya za watanzania waishio Mijini na Vijijini kwa kusogeza huduma za Madaktari bingwa karibu na Jamii .
Huduma za kibingwa zinazotolewa ni pamoja na Huduma za Afya kwa watoto na watoto wachanga,Huduma za Afya za uzazi ,wajawazito na magonjwa ya wanawake,Huduma ya Magonjwa ya Ndani(shinikizo la damu,Kisukari nk.,Huduma za upasuaji wa mfumo wa mkojo,Huduma za ganzi na usingizi,Huduma bingwa za kichwa na meno,Huduma bingwa za wauguzi Pamoja na Huduma bingwa za mifupa.
Mkoa wa Mtwara umepokea jumla ya Madaktari Bingwa 64 ambao wameweka Kambi katika Halmashauri 9 za mkoa wa Mtwara na watafanya kazi Kwa muda wa wiki Moja kuanzia tarehe 16-22,2024
# RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN ANAJALI AFYA YAKO, JITOKEZE KITUO CHA AFYA KITANGARI UPATE HUDUMA ZA AFYA ZA KIBINGWA KWA GHARAMA NAFUU#
@wizara_afyatz
@samia_suluhu_hassan
@mtwarars_habari
@dc_newala
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa