• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Newala District Council
Newala District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Newala

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko
      • Ukubwa wa eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya viongozi
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ujenzi
      • Planning, Statistics and Coordination
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • KIlimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • ICT & Public Relations
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Usambazaji
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
      • TASAF
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba

Tani 12,181 zauzwa kwenye mnada wa kwanza wa Korosho Newala

Posted on: October 31st, 2019

Wakulima wa Korosho Wilaya ya Tandahimba na Newala leo wameuza Korosho zao tani 13,181 kwa bei ya juu ya shilingi 2,526 kwa kilo moja huku bei ya chini ikiwa shilingi 2,468 kwenye mnada wa kwanza wa chama Kikuu cha Ushirika TANECU uliofanyika Mjini Newala.

Taarifa ya makusanyo ya Korosho na kiasi kilichoingizwa katika mnada iliyosomwa na Meneja Mkuu wa TANECU LTD Bw. Mohammed Nassoro  imebainisha kuwa korosho zilizouzwa zilikuwa kwenye maghala makuu ya TANECU LTD yaliyopo Newala na Tandahimba na Agrofocus Newala. Aidha kwenye ghala  la Agrofocus zimeuzwa tani 194, ghala la TANECU Newala zimeuzwa tani 6,303 na ghala la TANECU Tandahimba zimeuzwa tani 6,682.

Wakulima walifikia maamuzi ya kuuza korosho zao baada ya Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania, Frances Alfred kutoa taarifa ya bei ya korosho kwenye soko la duniani hadi kufikia leo kuwa kilo moja ya korosho inauzwa kati ya shilingi 2,440 hadi shilingi 2,740.

Mnada wa leo ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa ambaye amewasisitiza viongozi wa chama Kikuu cha TANECU LTD na Bodi ya Korosho Tanzania kuharakisha mchakato wa malipo ili wakulima walipwe fedha zao kwa muda muafaka.

Aidha kampuni 28 zilijitokeza kuomba kununua korosho ambapo hitaji lilikuwa kununua Korosho tani 40,000 lakini makusanyo ya korosho na kiasi kilichoingizwa katika mnada hadi kufikia Oktoba 29, mwaka huu kilikuwa tani 13,181 tu.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -HALMASHAURI YA WILAYA YA NEWALA December 29, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILII WA MAHOJIANO January 06, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2021 MNYAMBE SEKONDARI July 10, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 22, 2022
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • RAIS SAMIA AMEBORESHA SEKTA YA ELIMU NEWALA DC

    March 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA KINYWA NA MENO WAHUDUMIA WAGONJWA 319 NEWALA DC

    March 24, 2025
  • MIAKA 4 YA RAIS DKT. SAMIA SALUHU HASSAN AMEBORESHA HUDUMA ZA AFYA

    March 19, 2025
  • NEWALA DC YANUFAIKA NA JENGO LA UTAWALA,WATUMISHI

    March 18, 2025
  • Ona Zote

Video

Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Historia ya Halmashauri
  • Idara ya Rasilimali Watu

Kurasa mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Poralg
  • Secretariet ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Newala

    Anuani ya Posta: P.O. Box 16

    Simu: +255232410251

    Mobile:

    Barua pepe: ded@newaladc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma zetu

Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa