Mkuu wa Wilaya ya Newala Bi. Aziza Mangosongo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bw. Gelasius Byakanwa jana tarehe 30 Januari, 2019 amekabidhi zawadi ya pikipiki kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kitangari B ikiwa ni pongezi kwa shule hiyo kuongoza kwa ufaulu kimkoa katika matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2018.
Tukio hilo la kukabidhi zawadi hiyo ya pikipiki limefanyika kwenye mkutano wa baraza la madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Akikabidhi zawadi hiyo, Bi. Mangosongo amezitaka shule nyingine kuiga mfano wa shule ya msingi Kitangari B na kuhakikisha wanafunzi wanajifunza vizuri na kufanya vizuri katika mitihani yao na kwa Kitangari B pikipiki hiyo iwe ni motisha ya wao kuendelea kufanya vizuri zaidi.
Hali ya ufaulu katika mitihani ya Taifa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Newala imekuwa ikiongezeka kutokana na kuimarika kwa mikakati ya taaluma na utendaji kazi wa walimu, ambapo kwa upande wa darasa la saba hali ya ufaulu imeongezeka kutoka asilimia 65 kwa mwaka 2017 hadi asilimia 84 kwa mwaka 2018 sawa na ongezeko la asilimia 19.
Shule ya msingi Kitangari B imeshika nafasi hiyo ya kwanza kati ya shule 247 za msingi za Mkoa wa Mtwara zenye wanafuzi zaidi ya 40 zilizofanya mtihani wa taifa wa darasa la saba kwa mwaka 2018 kwa wanafunzi wake wote 49 kufaulu mtihani huo.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa