Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya Kusini leo imeanza rasmi mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa Nest kwa watendaji wa kata na vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Mafunzo hayo yamefunguliwa na Kaimu Afisa Utumishi wa halmashauri hiyo, Ndugu Christopher Kihindo, ambaye amewapongeza PPRA kwa kuandaa mafunzo hayo muhimu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi, Meneja wa PPRA Kanda ya Kusini, Ndugu Fenias Manasseh, alisema kuwa lengo la mafunzo ni kuwawezesha watendaji na wadau wengine kuelewa na kutumia mfumo wa Nest kwa ufanisi, ili kuboresha usimamizi wa ununuzi wa umma na kuongeza uwazi katika mchakato huo.
“Mfumo huu unarahisisha taratibu za ununuzi wa umma kwa kuimarisha uwazi, uwajibikaji, na ufanisi. Ni muhimu kwa wadau wote, wakiwemo watendaji wa serikali za mitaa,makundi maalum , wazabuni, na wafanyabiashara, kuhakikisha wanaufahamu ili kutumia fursa zilizopo,” alisema Manasseh.
Mafunzo haya yanahusisha makundi mbalimbali, yakiwemo makundi maalum, wafanyabiashara, wazabuni, watumishi wa umma kama walimu na watumishi wa afya ambapo kila kundi litapata mafunzo kwa siku moja,kuhakikisha kuwa wanapata uelewa wa kutosha kuhusu matumizi ya mfumo wa Nest.
Mafunzo haya yanatarajiwa kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa ununuzi wa umma katika halmashauri, kuhakikisha kuwa michakato inafanyika kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa.
@ortamisemi
@mtwarars_habari
@msemajimkuuwaserikali
@samia_suluhu_hassan
@newalafmtz
@dc_newala
@ppra_tanzania
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa