NEWALA
Halmashauri ya Wilaya ya Newala imetambulisha rasmi mradi wa Ujenzi wa Shule Mpya ya sekondari ya Mtunguru wenye thamani ya shilingi milioni 560.5 ili kuondoa changamoto ya wanafunzi kusafiri umbali mrefu kwenda kupata Elimu shule ya sekondari makukwe iliopo kata ya Makukwe.
Kaimu Afisa Elimu Sekondari Ndugu Rashidi Mnuwone aliwasilisha taarifa ya mapokezi ya fedha hizo kwa wananchi kwenye mkutano wa Kijiji uliofanyika julai 18,2024 Kijiji cha Mtunguru kata ya Mtunguru na kueleza kuwa kwa mujibu wa muongozo kutoka serikali fedha hizo zitatumika kujenga madarasa 8,Jengo la utawala,maabara za masomo ya sayansi 3,vyoo matundu 8,kichomea taka ,Jengo la maktaba na jengo la Tehama kwa ajili ya wanafunzi kujifunza teknolojia ya habari na mawasiliano.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Newala Ndugu Duncan Thebas amewaomba wananchi wa kata ya Mtunguru kujitolea nguvu kazi, kushirikiana na Serikali katika kujenga na kukamilisha mradi huo.
Aidha amempatia sifa Diwani wa kata hiyo Mhe.Rashid Ndembo kwa kuwaletea maendeleo wananchi wake .
Wananchi wa kata ya Mtunguru akiwemo Bi Lukia bakari na Kazumari Jazari na Diwani wa kata higo Mhe.Rashid Ndembo wamemshukuru Rais Samia suluhu kwa kuleta fedha za kujenga sekondari kwani watoto wao wataondoa adha ya kusafiri umbali mrefu kwenda kata ya Makukwe kupata Elimu.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa