NEWALA, MTWARA
Baraza la Madiwadi Halamshauri ya Wilaya ya Newala limefanya kikao cha kawaida,robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2024/25 Oktoba 24,2024 ambapo masuala mbalimbali yamejadiliwa katika taarifa za kamati za kudumu za Halamashauri,taarifa za maendeleo ya kata na miradi ya maendeleo.
Akifunga kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Mfaume Lada amesisitiza suala la utawala bora kwa watumishi wa umma katika kuwahudumia wananchi.
"Niendelee kusisitiza suala la Utawala bora,wananchi wamekuwa wakienda ofisi za vijiji,kata na maeneo mengine ya kupata huduma za kijamii lakini lugha wanazokutanazo sio lugha rafiki”
“kwa hiyo niombe watumishi wa umma kuhakikisha wananchi wenye matatizo wanasikilizwa na kuhudumiwa bila vikwazo na kama changamoto imezidi uwezo wa kushughulikia basi tumia njia ya ushirikishwaji kwa kuwatumia viongozi wa ngazi ya juu lengo ni kuona wananchi wanapata huduma bora” Amesema Lada.
Aidha ametoa rai kwa viongozi wa Halmashauri kuhakikisha miradi yote maendeleo inayotekelezwa ndani ya Halmashauri inasimamiwa na kutekelezwa kwa wakati na kwa ubora unaokubalika, kwani serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inawekeza fedha nyingi kwa ajili ya miradi hiyo.
Kwa upande wa Kaimu Mkurungezi Ndg. Mohamed Muhudini amewaomba madiwani kushiriki uchanguzi wa serikali za mitaa kwa kuhamasisha wananchi kuchagua viongozi bora ifikapo tarehe ya uchaguzi Novemba 27,2024 ambao watasimamia maendeleo katika vijiji na vitongoji..
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa