NEWALA, MTWARA
Mbunge wa Jimbo la Newala vijijini Mhe. Maimuna Mtanda amesema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Newala imepokea fedha shilingi Milioni 170.5 za mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kuchochea miradi ya maendeleo katika Jimbo la Newala Vijijini.
Mhe Mtanda amesema hayo kwa nyakati tofauti wakati akiwasilisha kitabu alichokiandika cha ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 kwa Wajumbe wa Mkutano mkuu wa Jimbo wa Tarafa ya Chilangala na Kitangari Julai 9,2014 ambacho kinaelezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo zilifanywa na Serikali na Mbunge Mtanda kwa wananchi wa Jimbo la Newala vijijini.
Amesema kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 shilingi Milioni 41.5 zilipokelewa, Mwaka 2022/2023 Milioni 64.5 zimepokelewa na Mwaka 2023/2024 shilingi Milioni 64.5 zimepokelewa na fedha zote zimetumika kwa malengo yaliyokusudiwa kwa kupeleka fedha na vifaa kama vile saruji na bati kwenye miradi ya vijiji vya kata zote za Newala vijijini.
" Hapa naomba nitoe ufafanuzi wa fedha za mfuko wa jimbo, kwanza hairuhusiwi kutumia fedha hizi kwa shughuli za kisiasa na shughuli za kidini"
" Pia fedha za mfuko wa jimbo hutolewa mara moja Kwa mwaka na kupelekwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na mgao wa fedha hizo hufanywa na Kamati ya mfuko iliyoundwa kwa majibu wa Sheria" amesema Mtanda
Aidha amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha hizo kwani zimesaidia kuchochea maendeleo Jimbo la Newala vijijini.
Mfuko wa kuchochea maendeleo ya Jimbo ulianzishwa mwaka 2009 kwa Sheria NA. 16 ya Mwaka 2009 ili kusaidia kuchochea maendeleo kwenye majimbo kwa kutekeleza miradi midogo midogo iliyoibuliwa na Wananchi kwenye Vijiji na Kata.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa