Mfuko wa elimu ni moja kati ya vyanzo vya mapato vilivyoanzishwa na Halmashauri ya Wilaya ya Newala ukiwa na lengo la kutatua changamoto za elimu hasa miundombinu yake kwa wilaya ya Newala. Mfuko huo unachangiwa na wakulima, wafanyakazi na wananchi wanaoishi kwenye eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Newala kusaidia kupunguza matatizo yanayoikabili sekta ya elimu yakiwemo Kupitia baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Newala la tarehe 24/04/2017, mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Chitwanga Rashidi Ndembo, aliwaambia wananchi kuwa michango ya wakulima wa zao la korosho kwa mwaka 2017, Halmashauri ya Newala imeweza kukusanya jumla ya shilingi 303,880,040.00 za mfuko wa elimu. “Mfuko huu una umuhimu sana kwa kuwa sekta ya elimu ina changamoto nyingi zikwemo ujenzi wa vyoo, madarasa, nyumba za walimu, ofisi za walimu na miundombinu yote inayohusu elimu” alisema Mhe. Ndembo. Na kwa kuzitatua changamoto hizo kiwango cha elimu kinakua na kuzalisha wasomi wengi kwa maendeleo ya Newala na taifa kwa ujumla.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa