No noKaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Ndg Magreth Likonda Leo tarehe 14-9-2023 amepokea vifaa vya ufundi uwashi kutoka makao makuu VETA vilivyodhaminiwa na TANPACK vifaa vyenye thamani ya Tsh. milioni 42.Pia kaimu Mkurugenzi mtendaji alikabidhii vifaa hivyo kwa vijana ambao walipata mafunzo ya utengezaji wa vihenge vya kuhifadhia nafaka.Makabidhiano hayo yamefanyika katika jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Aidha Ndg Likonda amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kupunguza changamoto ya ajira kwa vijana na kuomba vijana watumie fursa hii Ili kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wa Katibu wa udhibiti wa sumu kuvu Ndg: Azizi Mohammed amesema"vifaa hivi vimetolewa kwa lengo la kutengeneza vihenge vya kuhifadhia nafaka ili kudhibiti sumu kuvu na kuwaomba vijana wa Wilaya ya Newala wajitume Ili kila mmoja wao awe mfano Kwa wengine.
Pia vijana kwa pamoja wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MH: Samia Suluhu Hassan na kupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala kwa kuwajali na kuwapa fursa hii.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa