MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI ngazi ya kata Jimbo la Newala Vijijini Jana Januari 21,2025 wamekula kiapo cha maadili ili kuhakikisha kwamba wanafanya kazi yao kwa uadilifu, uwazi, na kwa kufuata sheria na taratibu zinazohusiana na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya mwanzo Kitangari Bi. Rozzy Jamila ambaye ameongoza zoezi hilo amesema kiapo hicho kinawataka maafisa hao kufanya kazi bila upendeleo, rushwa, au kuegemea upande wowote wa kisiasa,kuwajibika kwa vitendo vyao, kuhakikisha kwamba wanaheshimu na kufuata sheria .
Pia kuhakikisha kwamba maamuzi yote yanayofanywa wakati wa uandikishaji yanazingatia haki za kikatiba za wapiga kura na kutojihusisha na vitendo vinavyoweza kuathiri uaminifu wa mchakato wa uboreshaji wa daftari la wapiga kura .
Maafisa waandikishaji wasaidizi 22 ngazi ya kata katika Jimbo la Newala Vijijini wameanza mafunzo yao Jana Januari 21,2025 kuhusu Uboreshaji wa Daftari la wapiga kura na mafunzo hayo yatamalizika leo januari 22,2025 yakiongozwa na wataalam wawezeshaji kutoka Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi kwa kushirikiana na maafisa waandikishaji ngazi ya Jimbo .
# Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni Msingi wa Uchaguzi bora#
@ortamisemi
@mtwarars_habari
@tumeyauchaguzi_tanzania
@dc_newala
@msemajimkuuwaserikali
@newalafmtz
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa