Leo tarehe 31/01/2022,Meneja wa Wakala wa usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) Wilayani Newala Mhandisi Nsajigwa Sadiki ametenbelea na kujionea mradi wa maji Mnima ambao unatekelezwa na Mkandarasi SEBA CONSTRUCTION & DRILLING LTD ya Dar Salaam kwa gharama ya Tsh milioni 270.7
Akizungumza na wananchi wa Mnima , Mhandisi Nsajigwa amesema tayari Serikali imetoa Kiasi cha Shilingi Milioni 270.7 ambazo zitatumika katika ujenzi wa mtandao wa mabomba mita 11320,ukarabati wa matenki 2 ya Lita 250,000 na 45,000 na ujenzi wa vilula 7 vya kuchotea maji.
Amesema vijiji vitakavyonufaika ni pamoja na Mnima, Mnyambe,Bahati,Majembe juu na Hengapano,ambapo watu wapato 8437 wapata huduma ya maji safi na Salama.
Aidha Mhandisi Nsajigwa ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri wa maji Jumaa Aweso kwa jitihada za kuleta fedha za utekelezaji wa mradi huo.
Naye Fundi mkuu wa Seba Construction & Drilling ltd ,Franco Chungwa amesema wamejipanga kuhakikisha mradi huo unakamilika mapema kabla ya miezi 6 ya mkataba uliosainiwa.
Aidha kwa upande wa wananchi wa Kijiji cha Mnima wakiongozwa na Diwani wa kata ya Mnyambe, Fabian Mahanyuka wamefurahishwa na juhudi zinazofanywa na serikali za kutatua kero ya maji,lakini pia amewataka wananchi kushirikiana katika shughuli za kujitolea kuchimba mitaro na kutunza miundombinu ya maji .
Mradi wa maji Mnima uliibuliwa na wananchi wa Kijiji cha Mnima kwenye mkutano mkuu wa Kijiji uliofanyika mwaka 2019,na pia ni miongoni mwa miradi mitatu ya maji ambayo inatekelezwa wilaya ya Newala kupitia programu ya maji na usafi wa mazingira vijijini.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa