Katika kuhakikisha usafi wa mazingira unazingatiwa na kuleta manadiliko chanya katika Jamii ,Kitengo cha Mazingira na taka ngumu Halmashauri ya Wilaya ya Newala leo Desemba 13,2024 kimeongoza zoezi la usafi eneo la soko kuu Kitangari kwa kushirikiana na Uongozi wa serikali ya Kijiji na wafanyabiashara.
Zoezi hilo la usafi limesimamiwa na Afisa Afya na Mazingira Bi. Merry Chilemba pamoja na Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Kitangari Ndugu Mohammed Ajari ambapo wamehamasisha wafanyabiashara kufanya usafi eneo la soko ili kuzuia milipuko ya magonjwa inayotokana na uchafuzi wa mazingira.
Bi Chilemba amesema mikakati yao ni kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa usafi, na kuweka mfumo wa kisheria wa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Aidha amesisitiza kila mjasiriamali na mfanyabiashara katika Soko Kuu la kitangari anatunza mazingira yake, na pia anatoa taka zake kwa njia bora na salama na kuzihifadhi katika maeneo yaliyoanishwa na serikali
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Cha kitangari Ndugu Mohammed Ajari ametoa wito kwa wafanyabiasha kuhakikisha jukumu la usafi na utunzaji wa mazingira linakuwa la kila mmoja katika eneo la soko kuu.
Aidha amewaomba Wafanyabiashara hao kushirikiana na serikali ya kijiji katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa vizuri.
"Serikali ya Kijiji itahakikisha kuwa vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya usafi, kama vile visanduku vya taka, vitakuwepo kwa wingi na vitatumiwa kwa manufaa ya Jamii ili Soko Kuu la kitangari liwe la mfano bora wa usafi wa mazingira" amesema Ajari.
@ortamisemi
@dc_newala
@newalafmtz
@wizara_afyatz
@mtwarars_habari
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa