KIKAO CHA TATHMINI YA UFAULU WA WANAFUNZI
12-02-2024 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala ndugu Duncan G.Thebas, kwa kushirikiana na Maafisa Elimu Msingi na sekondari ameongoza kikao maalum cha tathmini ya ufaulu wa wanafunzi kwa kushirikisha wadau mbalimbali.
Kikao hicho, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri, kimewaleta pamoja walimu wakuu, wakuu wa shule, wataaluma na waratibu wa elimu ngazi ya kata kwa lengo la kutathmini hali ya ufaulu wa wanafunzi na kujadili mikakati ya kuboresha matokeo ya kitaaluma kwa mwaka wa 2025.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi mtendaji amesema kuwa tathmini ya ufaulu ni muhimu katika kubaini changamoto zinazokwamisha maendeleo ya elimu na kuja na suluhisho muafaka. "Tunataka kuona watoto wetu wanapata elimu bora na kufaulu kwa viwango vya juu. Ushirikiano wa wadau wote ni muhimu katika kufanikisha hili,"
Kwa upande wake, Maafisa Elimu wa Halmashauri, , waliwasilisha takwimu za matokeo ya mitihani ya hivi karibuni, akionyesha maeneo yenye mafanikio na yale yanayohitaji maboresho. Wlibainisha kuwa baadhi ya changamoto zinazosababisha ufaulu duni ni pamoja na uhaba wa walimu, mazingira duni ya kujifunzia, na ushiriki mdogo wa wazazi katika masuala ya elimu.
Wadau wa elimu waliopata nafasi ya kuchangia walieleza matumaini yao kwamba hatua zilizopendekezwa zitasaidia kuinua viwango vya ufaulu na kuboresha elimu kwa ujumla.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa