Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala, Ndugu. Mussa Chimae amedhamiria kupunguza na ikiwezekana kuziondoa kabisa kero zilizopo kwa wananchi wa eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Akisisitiza dhamira hiyo katika mkutano wa baraza la madiwani wa robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2018/2019 uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala siku ya Jumanne 30/10/2018, Ndugu. Chimae ameeleza kuwa alitoa agizo maalumu kwa watendaji wote wa vijiji kuitisha mikutano maalumu kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi. Kero hizo zitapokelewa na kuwasilishwa katika ngazi ya kata ili kutafutiwa ufumbuzi na baadaye kuwasilishwa ngazi ya Halmashauri kwa ajili ya utekelezaji zaidi.
Pia Ndugu. Chimae amewataka maafisa tarafa wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala kuwasimamia watendaji wa vijiji na kata katika tarafa zao ili kutekeleza agizo hilo kwa ufanisi.
Aidha, ili kushughulikia kikamilifu kero za wananchi, Ndugu. Chimae ameanzisha utaratibu wa kutembelea kwenye vijiji kila mwezi akiongozana na wakuu wa idara na vitengo ili kuweza kutolea maelezo kero zote zilizoibuliwa na wananchi.
Utaratibu huu utapelekea kupunguza kero kwa wananchi na kuongeza uwajibikaji kwa watendaji wa serikali kwa kuwa kila mmoja atajitahidi kutekeleza majukumu yake kikamilifu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma inayotakiwa kikamilifu hivyo kutekeleza dhana ya utawala bora.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa