NEWALA, MTWARA
Kaimu Afisa Utumishi na Rasilimali watu Halmashauri ya Wilaya ya Newala Ndugu Andrew Nyumayo amesema huduma Afya zinapaswa kujikita zaidi katika kuhakikisha kila mtu anapata Lishe bora wakati wote wa maisha yake .
Nyumayo amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya Afua za Lishe kwa Watendaji kata na Maafisa Tarafa yaliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri leo Septemba 4,2024.
" Uwekezaji kwenye lishe kunaweza kusaidia Halmashauri kufikia lengo la huduma ya Afya kwa wote na malengo ya maendeleo endelevu"
"Nendeni mkahamasishe Jamii na kuwapa elimu ya kuzingatia ulaji sahihi wa lishe Bora" amesema Nyumayo
Ulaji wa Lishe bora husaidia mwili kukua vyema, kuujenga mwili lakini pia huimarisha kinga dhidi ya magonjwa.
Kwa upande wake Afisa Lishe Halmashauri ya wilaya ya Newala Bi. Christina Lukinisha amesema wameamua kuwajengea uwezo Watendaji kata na maafisa Tarafa kuhusu maana ya Lishe Bora na umuhimu wake ili wapate uelewa wa kutosha wa kwenda kutoa elimu kwa Jamii .
" Nawaomba elimu mliyopata mukaifanyie kwa vitendo ili udumavu uweze kuondoka kabisa na kupunguza akina mama wajawazito kujifungua watoto wenye uzito pungufu" amesema Bi. Christina
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa