Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa jana tarehe 2/6/2020 ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Newala kwa kupata hati safi ya ukaguzi wa hesabu za mwaka 2018/2019.
Pongezi hizo zimetolewa na Mhe. Byakanwa kwenye baraza maalum la madiwani la kupokea na kujadili taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali.
Katika ukaguzi huo wa hesabu za kuanzia mwezi Julai 2018 hadi mwezi Juni 2019, Halmashauri ya Wilaya ya Newala ilikuwa na jumla ya hoja 27, kati ya hizo hoja 13 zilipatiwa majibu na kufungwa, hoja 3 zilihamishiwa mamlaka ya maji vijijini (RUWASA) na hoja 11 sawa na asilimia 41 ya hoja zote zinaendelea kufanyiwa kazi.
Wakati huo huo Mhe. Byakanwa ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Newala kuongeza ubunifu kwa vyanzo vipya vya mapato ili iweze kujiendesha na kulipa madeni waliyonayo yakiwemo malipo ya waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Pia katika baraza hilo maalum, Mhe. Byakanwa alitoa tuzo ya Rais ya kuhifadhi mazingira kwa washindi watano waliopatikana kwa kuongoza kutunza na kuhifadhi mazingira vizuri katika maeneo yao.
Mhe. Byakanwa akikabidhi hati ya pongezi kwa washindi wa kwanza wa tuzo ya Rais ya kuhifadhi mazingira ambao ni shule ya sekondari Mmulunga. Waliopokea tuzo hiyo kutoka kulia ni mwalimu mkuu wa shule hiyo, Mhe. diwani wa kata ya Chiwonga na mtendaji wa kata ya Chiwonga
Washindi hao ni shule ya sekondari Mmulunga, shule ya sekondari Mkoma II, kikundi cha uhifadhi wa mazingira cha Umoja kilichopo kwenye kijiji cha Chiwonga, Kijiji cha Mitema pamoja na shule ya msingi Mtunguru ambao wote kwa pamoja wakipewa hati ya pongezi pamoja na fedha taslimu.
Baraza hilo maalum la madiwani lilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha walimu Kitangari.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa