Halmashauri ya Wilaya ya Newala yapata hati safi katika ukaguzi wa hesabu wa mwaka wa fedha 2017-2018
Taarifa hiyo imetolewa na Bw.Shadrack Mrema kwa niaba ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Mkoa wa Mtwara katika mkutano maalum wa baraza la madiwani la kupitia hoja za ukaguzi ulilofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala siku ya Jumamosi tarehe 18 Agosti 2019.
Bw. Shedrack Mrema (aliyesimama na kushika karatasi) akisaoma taarifa mbele ya mkutano wa baraza maalum la madiwani kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Mkoa wa Mtwara
Baraza hilo lilikuwa ni maalum kwa ajili ya kuipitia taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali pamoja na mapendekezo ya utekelezaji wa maoni ya kamati ya fedha na uongozi na ofisi ya taifa ya ukaguzi wa hesabu za serikali ilishukuru kwa ushirikiano walioupata kutoka kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala wakati wa ukaguzi wa mwaka wa fedha 2017/2018.
Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ya Wilaya ya Newala imepata hati safi (inayoridhisha) ya ukaguzi. Hati ya ukaguzi ni maoni ya mkaguzi yanayoelezea iwapo taarifa za fedha zinazokaguliwa zimetayarishwa kwa kutumia sera na sheria zinazohusika, kanuni, viwango na misingi ya hesabu za fedha zinazotumika.
Licha ya kupatikana kwa hati hiyo safi, Halmashauri ya Wilaya ya Newala kwa mwaka wa fedha 2017-2018 ilikuwa na jumla ya hoja za ukaguzi 64 kati ya hizo hoja 22 ni za miaka ya fedha iliyopita, hoja 42 ni za mwaka wa fedha 2017-2018 ambapo kati ya hizo hoja 26 ni za jumla na hoja 16 ni za miradi. Hoja zote zilijibiwa na mkaguzi aliweza kuhakiki majibu ya menejimenti na kufunga hoja 12. Hoja zilizobaki ni 30 kati ya hizo hoja 10 ni za kisera ambazo zipo nje ya uwezo wa Halmashauri kuzitekeleza, hoja 5 ni hoja taarifa na hoja 15 zilihakikiwa na mkaguzi wa hesabu kwa mwaka wa fedha 2018-2019.
Lengo la kufanyika kwa ukaguzi wa hesabu ni kumfanya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kutoa hati ya ukaguzi alioufanya dhidi ya hesabu za mwisho zilizotayarishwa na menejimenti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha husika.
Pia ukaguzi huo hufanyika ili kuona iwapo fedha zilizoidhinishwa na bunge na baraza la madiwani zimepokelewa na kutumika kama bajeti ilivyoidhinishwa, zimekusanywa inavyotakiwa na zimetumika katika maeneo yanayostahili kwa mujibu wa bajeti na kwa kufuata sheria na kwamba zimetumika kwa umakini unaozingatia manufaa yaliyotarajiwa.
Aidha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bw. Gelasius Byakanwa, Mkuu wa Wilaya ya Newala Bi. Aziza Mangosongo alitoa maelekezo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Newala kuhakikisha hoja zote zilizobaki zinafungwa kabla ya mwezi Disemba 2019 na taarifa ya utekelezaji inawasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara; kumtumia mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kupata ushauri juu ya taratibu za manunuzi ya umma kabla ya utekelezaji wa miradi na kuunda kamati za ukaguzi wa ndani kadiri ya muongozo.
Bi. Mangosongo pia aliitaka Halmashauri ya Wilaya ya Newala kuhakikisha inawaalika ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali na Mkuu wa Mkoa katika kamati za ukaguzi wa ndani; watumishi kuhakikisha wanazuia hoja kuliko kuacha ziandikwe ndipo wazijibu; kutumia vizuri fursa inayotolewa na ofisi ya hazina ya kutoa fedha za miradi ya kimkakati ili kuongeza mapato ya ndani; kuongeza juhudi katika kusimamia na kudhibiti vyanzo vya mapato ya ndani kwa kununua na kuweka mashine za kukusanyia mapato (POS) katika kila kijiji; na kuhakikisha inafanya vizuri maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Halmashauri ya Wilaya ya Newala ni moja kati ya Halmashauri 185 za Tanzania bara. Kwa mwaka wa fedha 2017-2018 ulioishia tarehe 30 Juni 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Newala ilitayarisha hesabu zake kwa kutumia mfumo wa kihasibu wa kimataifa wa sekta za umma (IPSAS), sheria za fedha za Serikali za mitaa namaba 9 za mwaka 1982 na marekebisho yake ya mwaka 2000, pia kwa kuzingatia miongozo, maagizo mbalimbali kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI na kuziwasilisha kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali mnamo tarehe 29 Septemba 2018.
Taarifa hiyo imetolewa na Bw.Shadrack Mrema kwa niaba ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Mkoa wa Mtwara katika baraza maalum la kupitia hoja za ukaguzi lililofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala siku ya Jumamosi tarehe 18 Agosti 2019.
Kikao hicho kilikuwa ni maalum kwa ajili ya kuipitia taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali pamoja na mapendekezo ya utekelezaji wa maoni ya kamati ya fedha na uongozi na ofisi ya taifa ya ukaguzi wa hesabu za serikali ilishukuru kwa ushirikiano walioupata kutoka kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala wakati wa ukaguzi wa mwaka wa fedha2017/2018.
Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ya Wilaya ya Newala imepata hati safi (inayoridhisha) ya ukaguzi. Hati ya ukaguzi ni maoni ya mkaguzi yanayoelezea iwapo taarifa za fedha zinzokaguliwa zimetayarishwa kwa kutumia sera na sheria zinazohusika, kanuni, viwango na misingi ya hesabu za fedha zinazotumika.
Licha ya kupatikana kwa hati hiyo safi, Halmashauri ya Wilaya ya Newala kwa mwaka wa fedha 2017-2018 ilikuwa na jumla ya hoja za ukaguzi 64 kati ya hizo hoja 22 ni za miaka ya fedha iliyopita, hoja 42 ni za mwaka wa fedha 2017-2018 ambapo kati ya hizo hoja 26 ni za jumla na hoja 16 ni za miradi. Hoja zote zilijibiwa na mkaguzi aliweza kuhakiki majibu ya menejimenti na kufunga hoja 12. Hoja zilizobaki ni 30 kati ya hizo hoja 10 ni za kisera ambazo zipo nje ya uwezo wa Halmashauri kuzitekeleza, hoja 5 ni hoja taarifa na hoja 15 zilihakikiwa na mkaguzi wa hesabu kwa mwaka wa fedha 2018-2019.
Lengo la kufanyika kwa ukaguzi wa hesabu ni kumfanya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kutoa hati ya ukaguzi alioufanya dhidi ya hesabu za mwisho zilizotayarishwa na menejimenti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha husika.
Pia ukaguzi huo hufanyika ili kuona iwapo fedha zilizoidhinishwa na bunge na baraza la madiwani zimepokelewa na kutumika kama bajeti ilivyoidhinishwa, zimekusanywa inavyotakiwa na zimetumika katika maeneo yanayostahili kwa mujibu wa bajeti na kwa kufuata sheria na kwamba zimetumika kwa umakini unaozingatia manufaa yaliyotarajiwa.
Aidha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bw. Gelasius Byakanwa, Mkuu wa Wilaya ya Newala Bi. Aziza Mangosongo alitoa maelekezo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Newala kuhakikisha hoja zote zilizobaki zinafungwa kabla ya mwezi Disemba 2019 na taarifa ya utekelezaji inawasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara; kumtumia mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kupata ushauri juu ya taratibu za manunuzi ya umma kabla ya utekelezaji wa miradi na kuunda kamati za ukaguzi wa ndani kadiri ya muongozo.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa