Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo ( wa pili kutoka kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Wilaya alipokata utepe kuashiria ufunguzi wa pikipik tayari kwa kukabidhi pikipiki hizo 22 kwa Maafisa Elimu Kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala tarehe 13/09/2018.
Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo amekabidhi jumla ya pikipiki 22 kwa Maafisa elimu Kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Katika hafla hiyo fupi iliyofanyika leo tarehe 13/09/2018 katika ofisi kuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Newala, Mhe. Mangosongo amesema Serikali imeamua kuwapatia Maafisa Elimu kata pikipiki hizo, ili kurahisisha utendaji wa kazi, kufika maeneo ya kazi kirahisi, pamoja na kusimamia swala zima la utoro shuleni kwa watoto, na kuhakikisha walimu nao wanafanya kazi yao ipasavyo.
Wakati wa kukabidhi pikipiki hizo, Mhe. Mangosongo amewaasa maafisa elimu kata hao kuzitumia pikipiki hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na Serikali, na si vinginevyo ili kuleta tija katika swala zima la utoaji elimu bure linaloendelea kutekelezwa na Serikala ya awamu ya tano.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Mussa, ametumia fursa hiyo kuwaagiza maafisa Elimu kata kuhakikisha wanasimamia shule zao vizuri, ili kuleta matokeo chanya katika shule zote, kwani tayari kila Afisa Elimu Kata ameshatoa takwimu ya umbali kwa shule zake na umbali kuelekea Wilayani, na taarifa imetumwa kwa wafadhiri wa mradi wa tusome pamoja, kwa lengo la kutoa huduma ya mafuta kwa kila mwezi kulingana na bajeti ya mradi.
Nao maafisa Elimu Kata waliopata pikipiki hizo, wameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwapatia pikipiki hizo, na kusema kuwa pikipiki hizo zitawasaidia sana kurahisisha utendaki wa kazi zao za elimu na kwamba hawatakuwa na kikwazo cha usafiri katika usimamizi na ufuatiliaji wa maendeleo ya Elimu katika shule zao.
Zoezi hilo limekuja baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Newala kupitia Idara ya Elimu kupokea jumla ya pikipiki 22 zilizofadhiriwa na mradi wa Tusome Pamoja ambao unafadhiri Mikoa saba hapa nchini ukiwemo Mkoa wa Mtwara.
Mkuuwa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangososngo akikabidhi pikipiki kwa mmoja kati ya Maafisa Elimu Kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala tarehe 13/09/2018 Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Baadhi ya pikipiki kati ya 22 aina ya HONDA zilizofadhiriwa na mradi wa Tusome Pamoja kabla ya kukabidhiwa kwa Maafisa Elimu Kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa