Mkuu wa Wilaya ya Newala, Mhe. Aziza Mangosongo ameendesha harambee ya ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Mtunguru B iliyopo kijiji cha Mtunguru, kata ya Mtunguru, Wilaya ya Newala.
DC Newala akihamasisha wananchi wakati wa zoezi la harambee, Alhamisi 10/01/2019 kijiji cha Mtunguru
Harambee hiyo ilifanyika siku ya Alhamisi, tarehe 10 Januari 2018 ambapo ilihudhuriwa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Newala, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Ndg. Mussa Chimae, wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Newala, Wahe. Madiwani, viongozi na wananchi wa kijiji cha Mtunguru.
Aidha harambee hiyo imefanikisha kupatikana kwa fedha taslimu pamoja na ahadi ya fedha na vifaa vya ujenzi ambapo vyote vina jumla ya shilingi milioni kumi laki tisa elfu tisini na tisa na mia mbili.
Harambee hiyo imekuja baada ya wananchi wa kijiji cha Mtunguru kuonyesha nia ya kuwa na shule ya msingi katika kijiji chao ambapo mpaka sasa shule hiyo ina madarasa matatu, ofisi za walimu mbili na matundu ya vyoo matano vilivyojengwa kwa nguvu ya wananchi ambao walichangia kupitia zao la korosho ambapo kila mkulima alikatwa shilingi therathini kutoka katika kila kilo moja ya korosho, michangi ya shilingi elfu mbili kwa kila kaya na fedha kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Newala shilingi milioni kumi na tano na shilingi milioni moja na nusu kutoka katika mfuko wa jimbo.
Majengo ya madarasa na ofisi yanayotumika katika Shule ya msingi Mtunguru B kwa sasa
Shule hiyo ilifunguliwa rasmi mwaka 2016 ambapo mpaka sasa ina jumla ya wanafunzi 170.
Mhe.Mangosongo amewapongeza wananchi wa kijiji cha Mtunguru kwa kuona umuhimu wa elimu na alisisitiza wazazi kuhakikisha wanafunzi wanaripoti shule katika kipindi hiki ambacho shule zimefunguliwa na kuacha visingizio vya kutokuwa na fedha za kuwanunulia mahitaji watoto wao kwa kuwa Serikali imeshalipa shilingi bilioni ishirini na mbili kwa wakulima wa korosho wa Wilaya ya Newala na waliobaki wanaendelea kulipwa.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa