NEWALA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Newala DC kimeshinda kwa asilimia 100 katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27,2024.
Katika uchaguzi huo wagombea 2675 wamechaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Uenyekiti wa Kijiji nafasi 107,Uenyekiti wa Vitongoji nafasi 302,wajumbe mchanganyiko nafasi 1410 na wajumbe wanawake nafasi 856 .
Kwa mujibu wa taarifa ya Matokeo iliyotolewa na Afisa Uchaguzi Ndugu Lukumbuso Mbwilo kwa niaba ya Msimamizi wa Uchaguzi Newala DC imesema CCM imeshinda nafasi zote za uongozi katika uchaguzi huo sawa na asilimia 100.
Aidha Viongozi hao wamekula kiapo cha maadili leo Makao Makuu ya Halmashauri mbele ya Hakimu Mkazi, Mahakama ya Mwanzo Newala Mjini Bi Elicy Mkonya.
@ortamisemi
@msemajimkuuwaserikali
@mtwarars_habari
@dc_newala
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa