Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Newala leo tarehe 09/06/2020 limefikia ukomo rasmi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Mussa Chimae akiwasilisha taarifa katika mkutano maalum wa kusitisha shughuli za baraza la madiwani leo tarehe 09/06/2020.
Akiwasilisha taarifa yake katika mkutano huo maalum wa kusitisha baraza la madiwani, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bw. Mussa Chimae amesema kuwa madiwani hao waliingia rasmi madarakani tarehe 25/10/2015 na baraza linaahirishwa leo ili kupisha mchakato mwingine utakaowapata madiwani wengine kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025. Hivyo majukumu yote ya baraza hilo wakati madiwani hawapo yatafanywa na menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Newala na maamuzi yote yatatolewa taarifa katika baraza la madiwani lijalo litakaloundwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo akizungumza katika mkutano maalum wa kusitisha shughuli za baraza la madiwani leo tarehe 09/06/2020 katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha walimu Kitangari.
Akizungumza katika mkutano huo maalum wa kuahirisha shughuli za baraza la madiwani, Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo amelipongeza baraza hilo kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mhe. Mangosongo amewaeleza madiwani kuwa wakati wanatekeleza majukumu yao kwa kushirikiana na wataalamu, walikuwa wanatekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.
"Tuna kitabu cha ilani ya Chama cha Mapinduzi kinachoelezea kila sekta na mambo yatakayotekelezwa na asilimia za utekelezaji wake, hivyo yote yaliyokuwa yanatekelezwa yamefuata maelekezo hayo." Amesema Mhe. Mangosongo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Mhe. Chitwanga Rashid Ndembo akifunga mkutano maalum wa kusitisha shughuli za baraza la madiwani
Akifunga mkutano huo maalum wa kusitisha shughuli za baraza la madiwani, mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Mhe. Chitwanga Rashid Ndembo amewashukuru waheshimiwa madiwani na watumishi wote kwa imani yao kwake na ushirikiano waliompa kwa muda wote madiwani walipokuwa madarakani na amewataka kuendelea kufuata sheria, taratibu na kanuni katika kila watakachokuwa wanakifanya.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa