Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Newala lililofanyika siku ya Jumatatu tarehe 29 Aprili 2019 limewapandisha vyeo, kuwathibitisha kazini na kuwabadilisha vyeo vya muundo watumishi 112.
Akizungumza kwenye baraza hilo la Madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Mhe. Rashidi Ndembo ameeleza kuwa kati ya watumishi hao 112, watumishi 96 wamepandishwa vyeo, watumishi 9 wamebadilishiwa vyeo vya muundo na watumishi 7 wamethibitishwa kazini.
Aidha jumla ya watumishi walimu 808 wamepandishwa vyeo na tume ya utumishi ya walimu (TSC) na kufanya idadi ya watumishi waliopandishwa vyeo kufikia 904 wakihusisha watumishi waliopo Halmashauri ya Mji na Wilaya ya Newala ambao waliwekwa kwenye bajeti kipindi Halmashauri hizo mbili zikiwa Halmashauri moja.
Maamuzi hayo yamefanyika kwa mamlaka iliyopewa Halmashauri ya kuajiri, kuteua, kupandisha vyeo na kuthibitisha kazini watumishi wake watakaoonekana kumudu kazi katika nyadhifa zao kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa umma Na. 8 ya mwaka 2002 kifungu 6(1) (b) kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 19 ya mwaka 2004, ikisomwa pamoja na kanuni Na. 6 ya kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003.
Watumishi waliopandishwa vyeo ni wale waliotengewa bajeti kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na waliobadilishwa kada ni walioidhinishwa katika ikama na bajeti ya mwaka 2018/2019.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa